Friday 18 September 2015

WEWE NI WA THAMANI KULIKO UNAVYOFIKIRI.

Mwananadamu yeyote maadamu  upo duniani unatakiwa kufahamu wewe haupo kwa bahati mbaya, bila kujali ulizaliwaje, mazingira unayoishi sasa yanakutafsiri vipi au watu wanasemaje juu yako bado ni muhimu ufike mahali pa kutambua wewe haupo kwa bahati mbaya bali kuwepo kwako Mungu amehusika.  Vyovyote unavyoamini iwe katika Mungu aliye hai na wa kweli ama vinginevyo lakini naomba nichukue fursa hii kuzungumza na wewe mambo machache yatakayo kufikisha mahali pa kuamini wewe ni kiumbe wa pekee katika dunia hii ya mwenyezi Mungu.

1. Mwanadamu umeumbwa tofauti na viumbe vingine. Kwa wale tunaoamnini katika Biblia,
    tunaelezwa wazi kwamba Mungu alimuumba mwanadamu kwa sura na mfano wake. Hii ni sifa
    moja kubwa inayotutofautisha na viumbe wengine.

2. Tumeumbwa kutawala, viumbe vyote duniani vinatawaliwa na mimi na wewe.